BARCELONA YAANZA KUTESTI ZALI UPYA KWA ANDER HERRERA

KLABU ya Barcelona ya nchini Hispania imefufua tena mpango wake wa kumnasa kiungo mkabaji wa Manchester United, Ander Herrela raia wa Hispania.

Barcelona ilichemsha katika mpango wa kumnasa kiungo huyo katika dirisha lililopita na hivi sasa inataka kukamilisha usajili wake mwezi Januari, mwakani.


Herrela amekuwa na wakati mgumu kupata namba katika kikosi cha kwanza kufuatia uwepo wa Nemanja Matic hivyo Barcelona wanataka kutumia nafasi hiyo kumnasa.

No comments