BARCELONA YAIKWANYUA OLYMPIACOS 3-1 …Juventus nayo yaicharukia Sporting Lisbon


Barcelona imeendelea kuchanua kwenye kundi D la Champions League baada ya kuifunga Olympiacos 3-1.

Dakika ya 11 Dimitrios Nikolaou anajifunga na kuizawadia Barcelona bao la kuongoza. Dakika ya 42 Gerard Pique anatolewa baada ya kupewa kadi ya pili ya njano, Barcelona wanabaki pungufu hadi mwisho wa mchezo.

Lionel Messi anaipatia Barcelona bao la pili kunako dakika ya 61 huku Lucas Digne akitupia la tatu dakika ya 60 kabla Olympiacos hawajapata goli la kufutia machozi mfungaji akiwa ni Dimitrios Nikolaou.

Juventus ikaifunga Sporting Lisbon 2-1 katika mchezo mwingine wa kundi D.

No comments