BAYERN MUNICH 'YAMFUKUA' MSTAAFU WAKE KUZIBA NAFASI YA CARLO ANCELOTTI


BAYERN MUNICH inatarajiwa kumtangaza kocha wake wa zamani Jupp Heynckes kuwa kocha mpya wa klabu hiyo kuziba nafasi ya Carlo Ancelotti aliyetimuliwa.
Kwa mujibu wa gazeti la Bild la Ujerumani, Jupp Heynckes mwenye umri wa miaka 72, anarejea kwenye klabu aliyoicha mwaka 2013 baada ya kuipa mataji kibao likiwemo la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Heynckes alitangaza kustaafu mwaka 2013 huku warithi wake wote akiwemo Pep Guardiola, wakishindwa kufikia mafanikio yake.
Bayern inataka huduma ya Heynckes angalau kwa msimu mmoja kabla hajaitafuta kocha mwingine.

No comments