BERBATOV ASEMA MESSI NI ZAIDI YA CRISTIANO RONALDO


Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Dimitar Berbatov amesema Lionel Messi ni bora zaidi kuliko Cristiano Ronaldo.

Licha ya yeye na Ronaldo kushinda pamoja taji la Premier League mwaka 2009, lakini Berbatov anasema Messi ni mchezaji bora wa kizazi hiki na pengine bora kwa vizazi vyote.

"Anaweza kufunga, kutengengeza nafasi, ni mchezaji aliyekamilika, pengine ni mchezaji bora kuliko yeyote yule. Kama utamuuliza mtu yeyote mwenye umri mkubwa kuliko mimi, atakuambia kuhusu Pele, Maradona au Puksas na Di Stefano.

"Lakini kwa kizazi changu ni Messi au Ronaldo. Ni wachezaji bora, lakini kuna kitu ndani ya Messi kinanifanya nitamke kwa nguvu 'Messi! Messi!' kila ninapoitazama Barcelona kwenye TV", anaeleza Berbatov.No comments