BI KIZEE AIBUKIWA GHAFLA NA DENZEL WASHINGTON NYUMBANI KWAKE

GWIJI wa filamu za mapigano nchini Marekani, Denzel Washington amemshangaza bibi kizee baada ya kuamua kugonga ghafla mlangoni kwake na kumtembelea bila taarifa.

Washington mwenye miaka 62 alikuwa kwenye mgahawa akiuliziwa namna ya kumpata mzee huyo wa miaka 86 Juanita Hubbard ambaye alikuwa akiishi karibu na eneo hilo.

Staa huyo alifanya uamuzi huo baada ya kugundua Juanita ni shabiki yake mkubwa mwenye shauku ya kutaka kukutana nae.

“Hii ni siku maalum ya wanawake wazee na kwangu, nimeona niitumie kwa kumtembelea Hubbard," alisema.

mshindi huyo wa tuzo ya Oscar ambaye alikuwa amevaa suruali ya jinsi nyeusi na fulana nyeupe wakati alipomtembelea bibi.

No comments