CANNAVARO ATAMBA "YANGA ITAFANYA KWELI LEO, HATUTAPAKI BASI"

BEKI mkongwe wa timu ya Yanga, Nadir Haroub “Cannavaro” amesema kuwa kikosi chao hakitacheza soka la kujihami katika mchezo wa leo dhidi ya mahasimu wao, Simba.

Cannavaro amesema kwamba wamepania kuhakikisha wanapata mabao katika mchezo huo ili kuipiku Simba, hivyo mbinu ya kucheza soka la kujihami haitakuwa na nafasi katika mtanange huo wa kukata na shoka.

“Mechi ya Ngao ya Hisani hatukushambulia sana, kwa kiasi kikubwa tulijihami, lakini mchezo wa kesho (leo), unahitaji matokeo zaidi kwasababu tunahitaji kurudi kwenye nafasi tuliyoizoea,” amesema Cannavaro.

“Kwanini tujihami, kwani Simba kuna kitu gani kigeni kwetu mpaka tuwaheshimu tupaki basi, tutashambulia mwanzo mwisho,” aliongeza beki huyo.


Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika mchezo  wa Ngao ya Hisani ambapo Simba ilishinda kwa mikwaju ya penati baada ya dakika tisini za awali kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

No comments