CARABAO CUP: WEST HAM YAITUPA NJE TOTTENHAM


Ubabe wa Tottenham Hotspur umezimwa na timu yenye msimu mbovu, West Ham United ambayo imeshinda 3-2 katika michuano ya Carabao Cup.

Matokeo hayo yamaanisha kuwa West Ham inatinga hatua ya robo fainali huku Tottenham ikifungasha virago na kuagana na michuano hiyo.

Tottenham itabidi ijilaumu yenyewe kwa kushindwa kulinda uongozi wa bao 2-0 hadi mapumziko kwa magoli ya Moussa Sissoko na Dele Alli yaliyokuja katika dakika ya 6 na 37.

Andre Ayew akaifungia mara mbili West Ham dakika ya 55 na 77 kabla Angelo Obinze Ogbonna hajafunga goli la ushindi kunako dakika ya 70.

No comments