CHAZ BABA AISUBIRI KOLABO NA CHRISTIAN BELLA


Mwimbaji wa dansi Chaz Baba amesema hana tatizo la kufanya nyimbo ya ushirikiano  na Christian Bella.

Mwimbaji huyo aliyasema hayo katika maongezi yake na Clouds FM kupitia kipindi cha ‘Weekend Bonanza’ ambapo akadai jambo hilo ni zuri na ni moja ya njia za kubadilishana uzoefu.

Alipoulizwa na mtangazaji Khamis Dacota iwapo yupo tayari kufanya kolabo na Christian Bella, Chaz akasema: “Nipo tayari sina tatizo lolote”.

Dacota akawaahidi wasikilizaji wake kuwa jambo hilo atalibeba kwa mikono yake mwenyewe ili kuhakikisha waimbaji hao wanatoa nyimbo moja ya pamoja.

No comments