CHIRWA ACHEKELEA KUIBAMIZA SIMBA SC... asema ilikuwa kiu yake ya muda mrefu

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa timu ya Yanga, Obrey Chirwa amesema kuwa kiu aliokuwa nayo ya kuifunga klabu ya Simba imekatika baada ya juzi kufanikiwa kuingia nyavuni katika mchezo huo wa watani wa jadi.

Chirwa tangu atue nchini mapema mwaka jana hajawahi kuifunga timu ya Simba hata bao la kuotea lakini juzi alifanikiwa kuifunga bao muhimu la kusawazisha katika kipindi cha pili.

Donald Ngoma na Amissi Tambe ndio wafalme wa mechi hizi lakini katika mchezo wa juzi wote walikosekana uwanjani kwasababu ya majeraha na jahazi la ushambuliaji likiwa chini ya Mzambia Chirwa ambaye hakufanya makosa.

“Kumalliza mkataba wangu bila kuifunga Simba lingekuwa sio jambo jema kwangu nim kitu amnacho nilipanga muda mrefu nashukuru kimetimia”alisema Chirwa.

“Hizi ni mechi maalumu ambazo kila mchezaji angepanda kufanya kitu kwa ajili ya klabu yake, ni mchuano wenye hisia kali za mashabiki na kila mmoja angetaka kuweka Historia” alimaliza.

Chirwa alifanikiwa kuifungia Yanga bao la kusawazisha basada ya Simba kutangulia kufunga kupitia kwa Shiza Kichuya ambaye ni mara ya tyatu mfululizo anafanikiwa kufunga kwenye mechi za watani.

No comments