CHRIS BROWN SASA ATAMANI KURUDIANA NA RIHANNA

RAPA Chris Brown amesema kuwa anaamini ipo siku atarudiana na aliyekuwa mpenzi wake wa siku nyingi, Rihanna na kurejesha penzi lao la zamani.

Brown amesema kwamba bado akili yake inaota kurejesha uhusiano wake na Rihanna ambaye walitengana baada ya kumshushia kipigo kikali mwaka 2013.

Pamoja na kuzama kwenye uhusiano na wapenzi wengine wengi lakini inadaiwa kuwa hajaweza kumtoa Rihanna kwenye moyo wake.


Mara kadhaa wamekuwa wakionekana pamoja lakini kwa masuala ya kikazi na wala hakuonekani dalili yoyote kuwa Rihanna anataka kumpa nafasi nyingine tena.

No comments