Habari

CRISTIANO RONALDO ATAKA REAL MADRID IMSAJILI WILLIAM CARVALHO

on

CRISTIANO RONALDO amtaka rais wa Real Madrid Florentino Perez amsajili   William Carvalho.
Mabingwa hao wa La Liga wamekuwa na mwanzo mbovu msimu huu chini ya kocha Zinedine Zidane.
Real Madrid tayari imejikuta iko  pointi saba nyuma ya vinara Barcelona baada ya michezo saba tu ya La Liga.
Real wanategemewa kuvunja benki na kuimarisha kikosi chao dirisha la Januari na lile la kiangazi na kwa mujibu wa jarida la usajili la Hispania, Don Balon, tayari Ronaldo ana pendekezo lake.
Don Balon inasema Ronaldo anataka Real imsajili Mreno mwenzake Carvalho mwenye umri wa miaka 25.
Carvalho anayeichezea Sporting Lisbon, kwa muda mrefu sasa amekuwa aking’ara kwenye ligi ya Ureno na mara kadhaa amekuwa akihusishwa na usajili wa kwenda Premier League.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *