DAU LA LIVERPOOL KUMWACHIA COUTINHO LAPANDA TENA... Barcelona sijui!

JITIHADA za klabu ya FC Barcelona kumpata kiungo mshambuliaji wa timu ya Liverpool, Philippe Coutinho zinaweza kugonga mwamba baada ya mchezaji huyo kupandishwa tena thamani yake ya mauzo.

Liverpool imeweka wazi kuwa haitakubali kumwachia kiungo wake huyo kwa dau linalopungua pauni mil 133.


Klabu ya Barcelona baada ya kushindwa kumnasa katika dirisha kubwa la usajili walipanga kukamilisha dili hilo mwezi Januari mwakani.

No comments