DAVIDO ASEMA AMEWASAMEHE WOTE WALIOMPAKAZIA KESI YA MAUAJI

MWIMBAJI maarufu Afrika, Davido amesema kwamba hana kinyongo na wote waliompakazia tuhuma za mauaji ya rafiki yake, Tagbo Umeike.

Davido amesema kuwa ameshawasamehe wote waliokuwa wakimshambulia kutokana na kifo cha rafiki yake huyo aliyekwenda pamoja na DJ Olu.

Mwigizaji wa kike, Caroline Danjuma alikuwa mtu wa kwanza kumshambulia Davido kuhusiana na kifo hicho.

Davido alipelekwa kwenye kituo cha polisi kuhojiwa kuhusiana na kifo cha Tagbo baada ya tuhuma hizo kuelekezwa kwake.


“Asante Yesu kwa hiki kilichotokea kwangu na mimi nawasamehe wote waliojaribu kueneza tarifa za uongo,” ilisomeka sehemu ya taarifa fupi iliyotumwa na staa huyo.

No comments