DOUBLE M PLUS KUTUMBUIZA BONANZA LA HARBOURS CLUB KURASINI


Kocha wa Dunia – Mwinjuma Muumin, Jumapili hii ataliongoza kundi lake la Double M Plus katika bonanza maalum litakalofanyika Kurasini.

Muumin ameiambia Saluti5 kuwa bonanza hilo litafanyika Haurbours Club kuanzia saa 9 alasiri.

Bonanza hilo litashirikisha michezo mbali mbali ikiwemo soka na kuvuta kamba lakini mwisho wa siku watu wote watatulizwa na burudani kutoka kwa Double M Plus.

No comments