EDWARD NKETIAH KINDA WA MIAKA 18 AIBEBA ARSENAL DHIDI YA NORWICH …Man City yapenya kwa matuta


Arsenal imetinga robo fainali ya Carabao Cup kwa kuifunga Norwich 2-1 katika mchezo uliolazimika kwenda hadi ‘extra time’.

Timu hizo zilitoka sare ya 1-1 katika dakika 90 za kawaida, lakini Arsenal wakaibuka vijogoo kwenye dakika 30 za nyongeza.

Kinda wa miaka 18 Edward Nketiah aliyeingia dakika ya 85, ndiye aliyeifungia Arsenal mabao yote mawili.

Katika mchezo mwingine, Manchester City ikapenya kwa mbinde dhidi ya Wolves kwa penalti 4-1 baada ua kutoka sare ya 0-0 ndani ya dakika 120.

Matokeo ya mechi zote za Carabao Cup
zilizochezwa Jumanne usiku ni:

No comments