FAOUZI GHOULAM WA NAPOLI KUTUA MAN CITY KUZIBA PENGO LA BENJAMIN MENDYMANCHESTER CITY inatajwa kuwa ipo mbioni kumsajili nyota wa Napoli ya Italia, Faouzi Ghoulam katika usajili wa dirisha dogo la Januari.
Ripoti kutoka Ufaransa zinasema Pep Guardiona anataka kumsajili Ghoulam kama mbadala wa beki Benjamin Mendy ambaye atakuwa nje kwa msimu mzima baada ya kuumia goti.
Ghoulam, nyota wa kimataifa wa Algeria, atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu na hivyo City inaamini itampata kwa bei poa mwezi Januari.


No comments