Habari

FERNANDINHO: RONALDO AU MESSI WA KAZI GANI MANCHESTER CITY?

on

MANCHESTER CITY haina haja ya kumsajili Lionel Messi,wala Cristiano Ronaldo, hii ni kwa mujibu wa kiungo   Fernandinho.
Kocha Pep Guardiola ametumia zaidi ya pauni milioni 200 dirisha la kiangazi kwa kusajili wachezaji wapya wakiwemo Kyle Walker, Benjamin Mendy, Bernardo Silva na Ederson.
Lakini Messi peke yake angeweza kuigharimu klabu hiyo zaidi ya kiasi hicho cha pesa kama City ingejaribu kumsajili staa huyo wa Barcelona.
Kiungo wa Manchester City Fernandinho anaamini klabu yake ina nguvu ya kiuchumi ya kuweza kumsajili Messi au Ronaldo lakini haoni kama jambo hilo lina tija.
“Wakati mwingine lazima uangalie kwanza vipaumbele vya klabu. Tuna nguvu ya kiuchumi, kila mtu anajua hilo, lakini vipaumbele ndiyo vitu vya kuzingatiwa,” anaeleza kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil.
“Je tunataka kumsajili mchezaji mmoja au kikosi chenye nguvu cha kutuwezesha kufikia malengo yetu? Wakati mwingine watu wanakosea na kuamini kuwa mchezaji mmoja anaweza kutimiza kila mahitaji ya timu”.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *