GENEVIEVE NNAJI SASA AINGIA ANGA ZA HOLLYWOOD

MODO wa filamu za maigizo nchini Nigeria, Genevieve Nnaji ameingia anga za Hollywood baada ya kufanya kazi na mastaaKate Beckinsale, Damon Idris na Gugu Mmbatha.

Genevieve ameshirikishwa kwenye baadhi ya maeneo ya filamu iitwayo “Farming” ambayo imeanza kurekodiwa nchini Uingereza na maeneo kadhaa ya Nigeria.

Filamu hiyo imeanza kurekodiwa mwezi Agosti, mwaka huu ikiongozwa na Mwingereza Adewale Akinnuoye Agbaje mwenye asili ya Nigeria.

Genevieve hivi karibuni aliachia filamu yake ya “Lion Heart” na amekuwa akishirikishwa katika kazi mbalimbali za filamu baada ya kuteka soko nchini Nigeria.


Staa huyo pia ameshinda tuzo ya mwigizaji bora wa kike akiwa na jumla ya filamu 80 alizowahi kucheza tangu alipoanza kazi ya sanaa.

No comments