GIGY MONEY ASEMA "HEMEDY PHD SIO LEVO YANGU"

MDADA mkali wa kunogesha video za muziki Bongo aliyeamua kutumbukia katika muziki, Gigy Money, amedai msanii Hemedy PhD sio levo zake kwasababu hana fedha.

Kauli ya Gigy Money inakuja baada ya hapo awali kuripotiwa kupishana kauli kwa wawili hao na Hemedy alipoulizwa na kipindi cha The Playlist cha Times Fm alijibu hawezi kumzungumzia Gigy.

Gigy akipiga stori na Bongo5, amesema kuwa yeye kwanza hamjui Hemedy na hana hadhi ya kuongea na yeye: “Hawezi kuwa na hadhi ya kuongea na mimi kwa sababu hana hela.”

Hemedy na Gigy wote wanajihusisha na vitu viwili katika tasnia ya burudani Bongo, Gigy anafanya muziki na video vixen, Hemedy muziki na uigizaji.

No comments