HABARI NJEMA KWA MOURINHO NA MANCHESTER UNITED YAKE

Kuelekea mchezo mgumu wa Premier League Jumamosi hii dhidi ya Tottenham, kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amenufaika kwa kuimarika kwa safu yake ya ulinzi.

Sentahafu Eric Bailly aliyekuwa majeruhi, anarejea uwanjani baada ya kuzikosa mechi dhidi ya Liverpool, Benfica, Huddersfield na Swansea.

Aidha, wachezaji Marcus Rashford na Ander Herrera ambao walipata majeraha madogo madogo, nao wako fiti kuivaa Tottenham.
No comments