HARRY KANE AZUA MAMBO, PEP GUARDIOLA AMJIBU MAURICIO POCHETTINO


Pep Guardiola amemuomba radhi kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino na kusema kwa hakika alieleweka vibaya.

Guardiola alimtibua Pochettino pale alipoitaja Tottenham kama timu ya Harry Kane.

Pochettino akajibu mapigo kwa kutoa shutuma kali huku akisema Guardiola ameikosea adabu Tottenham. 

Hata hivyo Guardiola amefafanua kwa kusema: "Nadhani Mauricio amenielewa vibaya. Nimesikitishwa sana. Sijawahi kumvunjia mtu heshima hata mara moja.

"Pengine naweza kujibu pale mtu anapoishambulia klabu yangu, lakini kamwe sikudhamiria kuivunjia heshima Tottenham au Mauricio.

"Labda Kiingereza changu kilikuwa kibaya, niliposema kuhusu timu ya Harry Kane ilikuwa ni kwasababu amekuwa akifunga magoli mengi. Naelewa wazi kuwa Tottenham sio timu inayomtegemea Harry Kane peke yake."
No comments