HATIMAYE MANGO GARDEN YAFUNGWA RASMI …wamiliki wakubali yaishe, waanza kuvunja ukumbi


Waendeshi wa ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni wamekubali yaishe na kuanza kuuvunja rasmi ukumbi huo.

Kwa misingi hiyo, shughuli za kawaida na burudani ndani ya Mango Garden zimebakia kuwa historia huku FM Academia ikijiandikia historia ya kuwa bendi ya mwisho kupiga ndani ya ukumbi huo.

FM Academia ilifanya onyesho Ijumaa iliyopita Mango Garden.

Waendeshi wa wa ukumbi ho waliweka zuio mahakamani ili Umoja wa Vijana wa CCM ambao ndiyo wanaomiliki eneo lote la kuanzia Mango Garden, Vijana Hostel hadi Vijana Social Hall wasiruhusiwe kuvunja eneo hilo, lakini mwisho wa siku wamekubali matokeo na kuuanza kuuboma taratibu huku wakiamisha mali zao.

Kwasasa hakuna tena huduma Mango Garden, si chakula wala vinywaji. Saluti5 imeshuduia jiko na kaunta zote zikiwa zimevunjwa, paa la jukwaa la burudani na mengine yote yametolewa. BYE BYE MANGO GARDEN.2 comments

wadudu wadogo said...

MIE SISHANGAI, NILISEMAGA KUDUNDA DUNDA KWA MAHARAGE NDIO KUIVA KWAKE

Unknown said...

Kwaheri mango garden😭😭😭😭😭