HATIMAYE NYOSHI AIFICHUA BENDI YAKE MPYA


Aliyekuwa rais wa FM Academia, Nyoshi El Saadat ameanza kuifichua taratibu bendi yake mpya inayotarajiwa kuitwa Bogoss Musica.

Kwa muda mrefu Nyoshi amekuwa chimbo  akifanya mazoezi ya nguvu na vijana wake kwaajili ya kuandaa nyimbo mpya.

Wiki hii Nyoshi amejitosa studio kwaajili ya kurekodi nyimbo zake mpya.

Aidha, kupitia ukurasa wake wa Facebook, Nyoshi ametupia tangazo linaloonyesha kuwa atakuwa na mahojiano na Clouds TV Jumamosi hii katika kipindi cha Mamaland.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mtangazaji wa  Mamaland, Khamis Dacota, kipindi hicho kitaruka Jumapili 22 Oktoba saa 11 jioni, tofauti na tangazo la Nyoshi linavyosema.

Katika tangazo hilo, Nyoshi amelisindikiza na maandishi makubwa ya Bogoss Musica.

Bogoss ina historia ndefu na Nyoshi kwani ndiyo bendi aliyokuwa akiitumikia nchini Kenya, kabla ya yeye na wenzake hawajatua Tanzania mwishoni mwa miaka ya 90 na kuanzisha FM Musica International chini ya mfanyabiashara Felician Mutta.


No comments