HOMA YA TANZANIA BAND FESTIVAL YAZIDI KUPANDA KAHAMA


Tamasha la muziki wa dansi lililopewa jina la Tanzania Band Festival linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa mji wa Kahama na vitongoji vyake

Tanzania Band Festival itaanza kurindima mjini Kahama Ijumaa hii Oktoba 6 katika Uwanja wa Taifa Kahama na kufuatiwa na show ya jijini Mwanza Oktoba 7 ndani ya Rock City Mall.

Bendi zitakazoshiriki maonyesho ya Mwanza na Kahama ni FM Academia, Twanga Pepeta, Msondo Ngoma, Malaika Music Band na B Band.

Mtangazaji maarufu wa Kahama FM Dj Rammy (pichani kulia) ameiambia Saluti5 kuwa mji wa Kahama kwa sasa Tanzania Band Festival ndiyo habari ya mjini.

“Kwa hakika Kahama inasubiri kwa hamu kubwa tamasha hilo la kipekee, Ijumaa hii mwelekeo utakuwa ni mmoja tu – Uwanja wa Taifa Kahama kushuhudia Tanzania Band Festival,” anaeleza DJ Rammy ambaye ni mmoja wa wana harakati wa muziki wa dansi.

No comments