HUSSEIN JUMBE AIBUKA NA WIMBO MPYA “MAKALI YA WEMBE HAYACHANJI KUNI”


Mwimbaji gwiji wa dansi Hussein Jumbe, kupitia kundi lake la Talent Band, ameibuka na wimbo mpya kabisa “Makali ya Wembe Hayachanji Kuni”.

Akiongea na Saluti5, Jumbe amesema tayari wimbo huo umeanza kupigwa kwenye kumbi mbali mbali inazotuimbuiza Talent Band.

“Ni wimbo mzuri, lakini nazidi kusoma mapokeo ya mashabiki juu ya kigongo hicho, nikishajiridhisha kuwa kimekidhi matakwa ya wapenzi wetu, basi tutaingia studio kuurekodi,” alisema Hussein Jumbe.


No comments