IDD MORRO ACHEKELEA MAISHA MAPYA RIVER ROAD MUSIC BAND


IDD Morro ambaye ni kati ya waimbaji mahiri wa muziki wa dansi, ameonekana kufurahia maisha akiwa katika bendi mpya ya River Road Music Band inayoongozwa na mkung;utaji ngoma mahiri Bongo, Chacha Tumba.

Hivi karibuni, Idd ambaye chimbuko lake ni bendi ya Moro International, aliipa kisogo bendi ya Kibaha Carnival akiwa na wanamuziki wenzie wengine wote waliokuwa wakiunda kundi hilo, kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni maslahi kiduchu.   

Akiongea na Saluti5, Idd amesema kuwa anajiona yuko huru zaidi wakati huu, hasa kutokana na kuridhika na ladha ya maslahi mazuri aliyoanza kuipata ndani ya bendi hiyo.

“Maisha sasa ni matamu ndani ya River Road tofauti kabisa na ilivyokuwa kule Kibaha Carnival Band, si unaona ndugu yangu naanza kutoka shavu na kitambi?” alisema Idd akimweleza ripota wetu huku akitabasamu kuonyesha furaha.

No comments