JB AIPONDA BONGOMUVI KIAINA… awafagilia wasanii wa zamani akiwaita “vijana wa kazi”

KATIKA hali inayojipambanua kuwa ni kama vile kukubali kwamba bongomuvi imeporomoka, nguli wa tasnia hiyo Jacob Stephen “JB” ameibuka na kusema kuwa ameimiss team ya wasanii waliokuwa wanaunda kipindi cha “Mambo Hayo”.

JB amesema kuwa amesema kuwa, ameimiss team hiyo kutokana na ukweli kwamba ilikuwa inakusanya vijana wakali ambao kazi zao hadi leo zimebaki kuwa historia kwa mashabiki wa maigizo na filamu Bongo.

“Kipindi hicho watu walikuwa wanafanya kazi bwana, unakuta mtu anakaa kuisubiri siku fulani tu kwa sababu ya mchezo wa runingani na kama huo mchezo utampita anaweza kujuta utafikiri amepoteza kitita cha fedha,” amesema JB.

“Inabidi watu, hasa vijana wa sasa wajiulize mara mbilimbili, wenzao tulikuwa tunapiga bao wapi, na kisha nao wajitengenezee mazingira mazuri zaidi ya kukubalika kwa kila mtu,” ameongeza.

No comments