JESSICA ALBA: MPANGO WANGU NI KUENDELEA KUZAA TU

STAA wa filamu mwenye mvuto wa kimapenzi, Jessica Alba amesema kuwa mpango wake ni kuendelea kuzaa ili awe na familia yenye watoto wengi.

Alba anatarajia kupata mtoto wa tatu akiwa na mume wake Cash Warren lakini bado mrembo huyo shauku yake ni kuendelea kuzaa.

Staa huyo amefikisha watoto wawili ambao ni Honor mwenye miaka 9 na Haven mwenye miaka 6.

“Huwa nafanya kazi zangu bila matatizo ninapokuwa na ujauzito hivyo sioni kitu cha kunizuia kuendelea kuzaa, nafurahia kumiliki idadi kubwa ya watoto,” alisema Alba.


“Nahitaji kuwa mwenye afya bora wakati wote kabla ya baada ya kufungua ili niweze kudumu malezi na kazi zangu,” aliongeza.

No comments