JINAMIZI LA SARE BADO LAISUMBUA AZAM FC

PAMOJA na kwenda kwa kujiamini katika mchezo wa ugenini, timu ya Azam FC imejikuta ikivutwa shati baada ya kulazimishwa sare ya mabao 1-1 na timu ya Mwadui.

Mechi hiyo ilichezwa juzi katika uwanja wa Mwadui Complex na kuishuhudia Azam FC ikiendelea kugandwa na jinamizi la sare.

Sare hiyo inafanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 12 ikiwa na jumla ya michezo sita hadi sasa kwenye Ligi Kuu Bara.

Katika mchezo huo bao la Azam FC limefungwa dakika ya tisa na nahodha Himid Mao "Ninja" kwa njia ya mkwaju wa Penalti baada ya beki wa kushoto Bruce Kangwa kuangushwa ndani ya eneo la hatari.


Azam ingeweza kujipatia mabao zaidi ya mawili katika kipindi cha kwanza kama mshambuliaji wake chipukizi, Yahya Zayd na Mbaraka Yusuph wangekuwa makini kutumia nafasi takribani tatu za kufunga mabao.

No comments