JOSE MOURINHO AANZA KUICHOKONOA REAL MADRID... adaiwa kumfukuzia Casemiro

KOCHA wa timu ya Manchester United, Jose Mourinho ameanza kuichokoza Real Madrid baada ya kuhusishwa kumtaka staa wake, Casemiro raia wa Brazil.

Mourinho amepanga kumfanya Casemiro kuwa mchezaji ghali zaidi duniani ili kurahisisha mpango wa kutua Old Trafford.


Hata hivyo, usajili huo ni vigumu kukamilika baada ya klabu hizo kuwa katika hali ya vuta nikuvute pindi linapokuja suala la kuuziana wachezaji.

No comments