Habari

JOSE MOURINHO AWAKATA MAINI MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED

on

JOSE MOURINHO amewaonya mashabiki wa Manchester United kuwa ni mapema mno kuanza kuota ubingwa au hata kumaliza kwenye ‘top four’ ya Premier Legue.
Manchester United imekuwa na mwanzo mzuri msimu huu hasa baada ya kuwanasa Romelu Lukaku na Nemanja Matic. 
Imeshinda mechi sita za Premier League na kutoa sare mchezo mmoja, iko nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa nyuma ya Manchester City kwa tofauti ya magoli.
Mourinho anasema: “Katika ligi nyingine unaweza kusema timu inayoanza na ushindi wa mechi sita na droo moja, inakwenda moja kwa moja kutwaa ubingwa.
“Lakini kwa England hiyo haina maana yoyote, unaweza hata usimalize katika nafasi nne za juu,”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *