JURGEN KLOPP HAONI MRITHI WAKE IWAPO ATATIMULIWA LIVERPOOL


Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp anaamini ni makocha wachache sana watakaoweza kufanya yale aliyoyafanya Anfield ndani ya miaka miwili.

"Kama watanifukuza sasa hivi, sidhani kama kuna makocha wengi watakaofanya kazi bora kuliko niliyoifanya," anaeleza Klopp katika mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Manchester United.

"Sidhani kwamba nimekamilika kwa kila kitu, lakini ni ngumu kupata suluhisho sahihi. Naamini kwa asilimia 98 mashabiki wa Liverpool wanaona tuko katika njia sahihi, tutafanikiwa. Ni kazi yenye heshima kubwa, ni kazi ngumu lakini ya kuvutia, ninafurahia kila sekunde yangu hapa".
No comments