JUSTIN BIERER ARUDIANA NA SALENA GOMEZ

MASTAA wa muziki Justin Bieber na Selena Gomez wameanza tena kuonekana pamoja katika kumbi za starehe nyakati za usiku, hali iliyoibua hisia kuwa huenda wawili hao wameamua kurejesha penzi lao kama zamani.

Penzi la wawili hao ni kama homa ya vipindi kwani mwaka 2013 ilionekana ndio mwisho wa uhusiano wao lakini mwaka mmoja baadae wakarudiana kabla ya kuja kutengana tena baadae.

Juzi wawili hao waeekana wakiwa pamoja na wenye furaha katika Studio za Selena zilizoko kwenye jiji la California.

Penzi la mastaa hao lilikuwa linatajwa kuwa ni mvuto zaidi na kuwaongezea mapato kupitia tenda za matangazo ya biashara ambapo mara nyingi walichukuliwa pamoja.  

No comments