Habari

KEVIN DE BRUYNE ASHUTUMU SERA ZA CHELSEA ZA KUWATOA WACHEZAJI KWA MKOPO

on

KEVIN DE BRUYNE ameshutumu utamaduni wa Chelsea wa namna ya kuwatoa wachezaji wake kwa mkopo na kusema kwamba hiyo ni sababu kubwa iliyomfanya aihame klabu hiyo. 
Staa huyo wa Manchester City  alijiunga na Chelsea siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la Januari 2012 lakini akaendelea kubakia  Genk ya Ubelgiji kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.
Baada ya kumaliza msimu kwa kishindo, akapelekwa Werder Bremen mwaka uliofuatia ambako nako aling’ara.
Lakini alipoanza kuitimikia Chelsea hakupewa nafasi ya kudumu na akaamua kuachana na klabu hiyo Januari 2014 na kujiunga na Wolfsburg ya Ujerumani kwa pauni milioni 18.
Baada ya kutakata Bundesliga, nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji akanunuliwa na Manchester City kwa pauni 55 na sasa ni mmoja wa wachezaji tishio Premier League na barani Ulaya kwa ujumla.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *