KHLEO KADARISHIANA ACHEKELEA "KITUMBO" CHAKE

MREMBO Khleo Kadarishiana ameonekana kufurahia ujauzito wake baada ya kuanza kuposti picha mitandaoni mara kwa mara akieleza kila hatua inayoendelea kwenye hali yake hiyo.

Staa huyo anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza baada ya kupewa ujauzito na rafiki yake wa kiume, Tristan Thompson.

Uhusiano wao ulianza mwezi Septemba 2016 lakini wamepeleka mambo haraka na kutarajia kupata mtoto wao wa kwanza.


Khleo amekuwa akianika kila kitu kinachoendelea katika penzi lao kupitia kipindi maarufu cha runinga cha Keeping up with Kadarshian”.

No comments