KIPIGO DHIDI YA YANGA CHAIWEKA KAGERA SUGAR KWENYE WAKATI MGUMU

USHINDI wa timu ya Yanga dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, unaweza kuhatarisha hali ya mambo katika kikosi hicho kinachotumia uwanja wake wa Kaitaba mjini Bukoba.

Klabu ya Kagera inakamata nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi mbili katika michezo yake sita iliyochezwa na kipigo walichokipata juzi kinazidi kuwaweka kwenye mazingira magumu.

Hivi karibuni kulikuwa na taarifa za kutaka kulifumua benchi zima la ufundi kufuiatia mwenendo mbaya wa timu hiyo lakini baadaye ilikuja kukanushwa.

Klabu ya Kagera imekuwa na kawaida ya kutovumilia vipigo kwani hata msimu uliopita walipopigwa bao 6-2 na Yanga kuliibuka tafrani kwenye kambi yake na kuanza kusaka mchawi wakiamini hakikuwa kipigo cha kawaida.


Katika mchezo wa juzi mabao ya Yanga yalifungwa na Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa ambaye ametoka majeruhi kwa muda mrefu.

No comments