KOBE BRYANT KUGEUKIA UJASIRIAMALI

STAA wa mchezo wa kikapu, Kobe Bryant amesema kuwa mpango wake ni kuwa mfanyabiashara mkubwa baada ya kupata mafanikio kupitia michezo.

Bryant hivi sasa anaongoza kampuni ya kutengeneza vinywaji kwa wanamichezo inayoitwa "Body Armor" lakini anahisi anatakiwa kufanya uwekezaji mkubwa ili afikie ndoto zake.

Kampuni hiyo inatarajia kufikia maono hayo mwaka 2025 baada ya kuanza kuteka soko la vinywaji baridi nchini Marekani.


“Nimeanza na vinywaji vya wanamichezo ambavyo huwasaidia kuwapa nguvu lakini bado kuna uwekezaji mkubwa unaendelea ili kufikia maono yangu,” alisema mkongwe huyo wa mchezo wa kikapu.

No comments