KOCHA SHAKESPEARE ATIMULIWA LEICESTER BAADA YA MECHI 10 TU ZA MKATABA WAKE MPYA


Kocha wa Leicester City, Craig Shakespeare ametimuliwa kazi baada ya kuiongoza timu hiyo katika mechi 10 tu ndani ya mkataba wake wa miaka mitatu aliosaini miezi minne iliyota.

Leicester City inashikilia nafasi ya tatu kutoka chini katika katika msimamo wa Premier League na hawajashinda mechi yoyote miongoni mwa mechi sita za mwisho walizocheza.

Shakesspeare mwenye umri wa miaka 53, alichukua mikoba ya Claudio Ranieri  mwezi Februari kwa muda lakini baada ya kuiongoza Leicester na kuweza kumaliza katika nafasi ya 12, alipewa mkataba wa kudumu mwezi Juni.

Shakespeare alishinda mechi 8 kati 16 akiwa mkufunzi wa timu hiyo msimu uliopita na kuisaidia klabu hiyo kufika katika robo fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Mara ya mwisho kwa Leicester kucheza mechi sita bila ushindi ilikuwa ni msimu uliopita ambapo Ranieri alifutwa kazi ikiwa ni miezi tisa tu baada ya kuisaidia timu hiyo kushinda taji la Premier League.

No comments