KOCHA WA TOTO AFRICANS MARUFUKU BENCHI LA UFUNDI

KOCHA wa timu ta Toto Africans, Almasi Moshi amezuiwa kukaa kwenye benchi la timu yake kutokana na kutokidhi matakwa ya kanuni ya 72 (3) ya Ligi Daraja la kwanza kuhusu benchi la ufundi.

Kwa mujibu wa sheria, kocha wa timu ya Ligi daraja la kwanza anatakiwa kuwa na Leseni ya chini kuanzia daraja C ya shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF.

Klabu hiyo pia imepigwa faini ya shilingi laki moja kwa kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ikiwa na maofisa watatu badala ya wanne wakati wa mechi namba 10 ya kundi C la Ligi daraja la kwanza dhidi ya Transit Camp FC iliyochezwa Septemba 29, mwaka huu katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Adhabu dhidi ya klabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 14(3) ya Ligi daraja la Kwanza kuhusu taratibu za mchezo na kitendo chao cha kuwa pungufu kwenye pre Match Meeting ni kukiuka kanuni ya 14(2b) ya Ligi daraja la kwanza.


Klabu ya Mvuvumwa FC pia imepigwa faini ya shilingi laki moja kwa kuhudhuria kikao cha maandalizi ikiwa na maofisa wawili tu baada ya wanne wakati wa mechi namba 5 ya kundi A la Ligi daraja la kwanza dhidi ya Kiluvya United iliyochezwa Septemba 22 mwaka huu katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

No comments