KOCHA WA ZAMANI WA SIMBA ATAMANI KUREJEA TENA MSIMBAZI

KOCHA wa zamani wa Simba, Goran Kopunovic amekiri kwamba anatamani kurejea Simba na kama angepata nafasi ya kutua tena katika kikosi cha Wekundu hao, angefanya makubwa zaidi.

Akiongea kwa njia ya simu kutoka nyumbani kwao nchini Serbia, Kopunovic amesema kwamba ingawa hajafanya mazungumzo na mtu yeyote katika Simba kwa sasa, lakini kama angepewa nafasi ya kurejea angetimiza kile ambacho hakumalizia alipokuwa Simba.

“Ni kweli kwamba kuna mambo nilipanga kuyafanya nilipokuwa Simba lakini sikuweza kuyakamilisha. Unajua niliondoka Simba nikiwa na lengo la kuisaidia timu, lakini kuna mambo yakatutenganisha,” amesema Goran.


Kocha huyo ambaye aliondoka Simba mwezi Mei, mwaka 2015, amesema anatamani kurejea kuifundisha timu hiyo kama itampa nafasi, ingawa amesema kwamba kufundisha timu za Afrika Mashariki kuna changamoto zake.

No comments