KOMBINESHENI YA AJIB NA CHIRWA YAMKUNA KOCHA LWANDAMINA

HABARI kubwa sasa Yanga sio ushindi bali ni kombinesheni ya mabao kati ya washambuliaji wawili Obrey Chirwa na Ibarahimu Ajib ambao kasi yao imewapa kiburi Wanayanga kuamini kwamba kazi ipo kwa mabeki wa upinzani.

Katika mchez0 wa pili sasa Ajib na Chirwa wameonyesha kuzoeana ambapo kombinesheni yao imempa kiburi kocha Geogre Lwandamina akisema wawili hao sasa wameiva na watakufa wengi.

Lwandamina amesema amefurahishwa na hatua ya washambuliaji hao wawili wanavyojua kusomana na kupeana pasi za mabao ambapo sasa anataka kuona wanazoeana zaidi.

“Ukiangalia huu ni mchezo wa pili wanafanya vizuri, wamekuwa na ushirikiano mkubwa sana wanapocheza kwa pamoja, wakiendelea hivi nafikiri hakuna timu itakayotoka salama, ni watu hatari sana,” alisema Lwandamina.

Kauli hiyo ya Lwandamina inakuja kufuatia Ajib kutangulia kumtengenezea Chirwa bao la kwanza kwa pasi yenye mandhari ya Ulaya lakini pia Chirwa akajibu mapigo kwa kumpigia bao safi Ajib akifunga la pili huku wote wakitoa pasi kwa mguu wa kulia na kufunga kwa kulia.

No comments