LEICESTER CITY YANYEMELEA SAINI YA BEKI BACARY SAGNA

KLABU ya Leicester City inavizia saini ya beki Bacary Sagna mwenye miaka 34, ili kuwaongezea nguvu msimu huu.

Sagna amewahi kuzichezea timu za Manchester City na Arsenal akiwa beki wa kulia na katika dirisha la Januari anaweza kujiunga na Leicester City.


Beki huyo anaweza kupatikana kirahisi kwa sababu kwa hivi sasa hajafungamana kimkataba na timu yoyote.

No comments