LIVERPOOL, ARSENAL ZAPIGANA VIKUMBO KUMWANIA KIUNGO WA MONACO

KLABU ya Liverpool na Arsenal zote za nchini England zimeingia vitani kumwania kiungo wa timu ya Monaco, Thomas Lemar.

Kiungo huyo mwenye miaka 21, anaweza kutua katika moja ya klabu hizo kwenye dirisha kubwa la usajili baada ya msimu huu kwisha akiwa ameonyesha nia ya kutaka kucheza England.


Katika vita hiyo, Arsene Wenger anaweza kufanikiwa kutokana na namna anavyoishi vizuri na raia wa Ufaransa ambao wanacheza chini yake.

No comments