LIVERPOOL YAZIDI KUJITENGA NA MBIO ZA UBINGWA ENGLAND


Ingawa ni mapema mno kusema lolote, lakini inaonyesha wazi kuwa Liverpool imeruhusu kudondosha pointi nyingi kwenye mbio za kusaka taji lao la kwanza Ligi Kuu ya England baada ya miaka 26.

Kikosi hicho cha Jurgen Klopp kimeambulia sare ya 1-1 licha ya kutawala mchezo wao dhidi ya Newcastle United kwenye uwanja wa St James Park.

Philippe Coutinho aliitanguliza Liverpool katika dakika ya 29 lakini Bizzare Joselu akaichomolea Newcastle dakika ya 36.


No comments