LWANDAMINA ASAKA STRAIKA ATAKAYEWAKIMBIZA CHIRWA, TAMBWE YANGA SC


YANGA inasaka kwa siri straika mchana nyavu na kwamba taarifa hizo zimeongeza ushindani kwa washambuliaji waliopo sasa hasa Obrey Chirwa na Amiss Tambwe.

Taarifa kutoka katika kamati ya usajili ni kwamba Yanga inafanya kazi kwa usiri mkubwa kutafuta mshambuliaji huyo na kwamba endapo mambo yatakuwa sawa utamu wa mabao utazidi kuliko sasa.

Bosi mmoja wa Yanga amesema kocha George Lwandamina amemtuma msaidizi wake Noel Mwandila kufuatilia kazi ya straika mmoja tishio ikiwa ni kazi ya siri ambapo kama msaidizi wake huyo atagundua bado mshambuliaji huyo yupo katika ubora jina lake litapelekwa kwa mabosi hao.

Ingawa jina la mshambuliaji huyo limekuwa siri kubwa lakini tetesi zinadai kwamba mchana nyavu huyo kwa sasa ni mfungaji bora akiongoza kwa kufunga mabao nane katika mechi nne za Ligi alizocheza.


Inaelezwa kwamba endapo mshambuliaji huyo atakubalika basi basi Chirwa ambaye mkataba wake unafikia ukingoni mwishoni mwa Desemba, mwaka huu, huku akigoma kuongeza mkataba au Tambwe anayekumbwa na majeraha kati yao mmoja anaweza kumpisha mchana nyavu huyo.

No comments