MADONNA AFURAHIA KUIONA URENO UWANJANI

MADONNA ambaye ni staa wa muziki wa Pop duniani, amesema kwake ilikuwa jambo la kipekee kuingia uwanjani na kuishuhudia timu ya taifa ya Ureno ikicheza mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia.

Madonna alinaswa na kamera uwanjani sambamba na mtoto wake wa kurithi, David Banda wakishuhudia mchezo kati ya Ureno na Switzerland.

Mtoto huyo wa Madonna yupo kwenye kituo cha soka kilicho chini ya klabu ya Benfica ya nchini Ureno.

Kinda huyo anayelewana na Madonna, anataka kufuata nyayo za staa wa dunia Cristiano Ronaldo ambaye anaichezea klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania.


Madonna ni mkongwe wa miondoko ya Pop lakini pia amekuwa akijihusisha na masuhala ya kulea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.

No comments