MADRID YAZIDI KUKOLEZA MOTO KWA HARRY KANE

KLABU ya Real Madrid inakoleza moto wa kumsajili mshambuliaji wa timu ya Tottenham Hotspurs, Harry Kane ambaye amekuwa moto kwenye kikosi hicho cha jiji la London.

Madrid imepanga kuweka rekodi ya usajili kwa kumtwaa mshambuliaji huyo kwenye dirisha dogo la Januari, baada ya kutofanikiwa katika dirisha lililopita.


Spurs waliwahi kumuuza Gareth Bale kwenda Madrid kwa ada iliyoweka rekodi na hivi sasa ada ya Kane inatajwa kuwa kubwa zaidi.

No comments