HUSSEIN JUMBE NA TALENT BAND WAENDELEA KUITAMBULISHA NYIMBO MPYA "MAKALI YA WEMBE"


Talent Band  chini ya nguli wa mwimbaji Hussein Jumbe “Mzee wa Dodo” kinaendelea kuutambulisha wimbo wake mpya "Makali ya Wembe" katika kumbi mbali mbali inazopiga.

Katika mazungumzo maalum na Saluti5, Jumbe amewaomba mashabiki kuhudhuria kwa wingi kwenye show zake ili wapate wasaa kukisikiliza live kigongo kipya cha bendi yake kabla hakijarekodiwa rasmi.

“Najua bado mashabiki wetu wanacharushwa na vibao kama Kiapo Mara Tatu, Pombe Nimeikosea Heshima na Dharau Zimezidi, lakini niwaambie tu kwamba tumewashushia zawadi ya kibao kipya  ‘Makali ya Wembe’,” amesema Jumbe.

No comments