Jeff Hendrick ameifungia Burnley bao pekee dhidi ya Everton kwenye mchezo wa Premier League uliochezwa Goodison Park na kuzidi kumweka pabaya kocha Ronald Koeman ambaye yupo kwenye shinikizo kubwa.

Everton imekuwa na mwendo mbaya msimu huu licha ya kufanya usajili mkubwa na sasa ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi baada ya kuambulia pointi saba tu katika michezo saba.

Hendrick alifunga bao hilo kunako dakika ya 21, akimalizia jumla ya pasi 24 zilizopigwa bila mchezaji yeyote wa Everton kugusa mpira.

Everton (4-2-3-1):Pickford 7; Martina 6.5, Keane 6, Williams 5, Baines 6; Schneiderlin 5 (Rooney 63mins 6), Gana 6; Calvert-Lewin 6.5, Sigurdsson 5, Vlasic 6 (Davies 69mins 6); Niasse 5 (Ramirez 82mins) 

Burnley (4-5-1): Pope 7; Lowton 7, Mee 8.5, Tarkowski 8, Ward 7; Brady 7.5, Defour 6.5, Hendrick 7 (Barnes 87mins), Cork 7, Arfield 7; Wood 7 

  
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac