MAN CITY YAILAMBA NAPOLI 2-1 … Feyenoord 1 - 2 Shakhtar Donetsk, Monaco 1 - 2 Besiktas, RB Leipzig 3 - 2 FC Porto


Manchester City imeendelea kutakata msimu huu baada ya kuinyoa Nopoli ya Italia 2-1 kupitia mchezo wa kundi F wa Champions League.

City ilimaliza biashara mapema kufuatia magoli ya Raheem Sterling dakika ya 9 na Gabriel Jesus dakika ya 13 wakati Napoli walipata bao lao la pekee dakika ya 73 kupitia penalti iliyopigwa na Amadou Diawara.


Feyenoord ikakubali kichapo cha 2-1 kutoka kwa Shakhtar Donetsk katika mchezo mwingine wa kundi F.

Kundi G matokeo yalikuwa kama hivi: Monaco ya Ufaransa ikachapwa 2-1 na  Besiktas ya Uturuki, RB Leipzig  ya Ujerumani ikaitandika FC Porto ya Ureno 3-2.

No comments